1 Chronicles 29:3-9

3 aZaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: 4 btalanta 3,000
Talanta 3,000 za dhahabu sawa na tani 110.
za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000
Talanta 7,000 za fedha ni sawa na tani 260.
za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu,
5kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?”

6 eNdipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000
Talanta 5,000 za dhahabu ni sawa na tani 190.
na darkoni 10,000
Darkoni 10,000 za dhahabu ni sawa na kilo 84.
za dhahabu, talanta 10,000
Talanta 10,000 za fedha ni sawa na tani 375.
za fedha, talanta 18,000
Talanta 18,000 za shaba ni sawa na tani 675.
za shaba na talanta 100,000
Talanta 100,000 za chuma ni sawa na tani 3,750.
za chuma.
8 kKila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 9 lWatu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

Copyright information for SwhNEN